Connect with us

Maisha

Trevor Noah anunua mjengo unaogharimu dola milioni 10

Trevor Noah, raia wa South Africa aliyekaimu nafasi ya Jon Stewart kama muongozaji wa kipindi cha “The Daily Show” mnamo 2015 amenunua apartment inayogharimu dola milioni kumi za kimarekani huko New York.

Apartment hiyo ambayo ipo ndani ya jengo la Stella (Stella Tower) ina vyumba vitatu vya kulalia ambavyo vipo katika ghorofa ya 17 na 18 ya jengo hilo.

 

Awali apartment hiyo ilitajwa kugharimu dola milioni 13 na baadae kushuka mpaka dola milioni 11.49 na kufikia makubaliano ya mauzo hayo hapo Jumatatu.

Trevor ni Muafrika wa kwanza kabisa kuwa muongozaji wa kipindi maarufu cha televisheni nchini Marekani , The Daily Show.

 

Continue Reading

More in Maisha

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top