Connect with us

Michezo

Mkongwe wa Arsenal Tony Adams ateuliwa kocha Granada

Nahodha wa zamani Arsenal Tony Adams

Nahodha wa zamani wa klabu ya Arsenal Tony Adams ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu kutoka nchini Hispania Granada.

Klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini humo La Liga imemteua Tony Adams kuziba nafasi ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Lucas Alcaraz ambaye alifungashiwa virago kutokana na mwenendo mbaya wa klabu hiyo

Adams atakuwa na kibarua kigumu cha kuiepusha Granada kushuka daraja ikiwa imesalia michezo saba tu kuelekea ukingoni mwa ligi hiyo.

Mara ya mwisho Adams kuongoza klabu kama kocha ilikuwa mnamo mwaka 2011 alipoinoa klabu kutoka Azerbaijani Gabala FC.

Adams alistaafu soka mnamo mwaka 2002 huku akioongoza klabu ya Arsenal kushinda mataji manne na makombe matatu ya FA, aliaanza maisha ya ukocha katika klabu ya Wycombe Wanderers mnamo 2013 na kisha kuhamia katika klabu ya Portsmouth hapo mwaka 2008. Alitumikia klabu ya Galaba FC zaidi ya mwaka mmoja na kisha kuondoka mara baada ya kuifikisha klabu hiyo nafasi ya saba, hata hivyo alirudi mwaka mmoja baadae kuwa mkurugenzi wa soka.

Continue Reading

More in Michezo

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top