Connect with us
Jeff Bezos

Biashara

CEO wa Amazon Jeff Bezos awa mtu tajiri duniani kwa muda mfupi

Mwanzilishi wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos kwa muda mfupi alimpita bosi wa Microsoft Bill Gates hapo Alhamisi na kuwa mtu tajiri zaidi duniani, kwa kuwa na thamani ya dola bilioni 91.4.

Kupanda kwa haraka kwa hisa za Amazon ndio ilikuwa sababu ya Jeff Bezos kumtoa kileleni mmiliki huyo wa Microsoft kwa masaa machache, Forbes ilisema.

Hisa za Amazon zilishuka baadae na kumfanya Bill Gates kurudi tena katika nafasi ya kwanza na kuwa mtu tajiri zaidi duniani.

Bezos mwenye umri wa miaka 53, anamiliki asilimia 17 za hisa za Amazon, na pia amekuwa akishughulika na biashara zingine.

Bezos na Gates wanapishana kidogo sana  na hivyo huenda hapo baadae boss huyo wa Amazon anaweza kumuondoa tena kileleni mmiliki wa Microsoft.

Continue Reading

More in Biashara

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top