Connect with us
Kevin Hart akitabasamu / tiririkablog.com

Mahusiano

Kevin Hart ajibu tuhuma za kumsaliti mkewe mjamzito

 

Mchekeshaji raia wa Marekani Kevin Hart amejibu tuhuma kuhusu kumsaliti mkewe alye mjamzito, Eniko Hart.

Katika taarifa iliyotolewa na Radar Online, Hart alirekodiwa video akimsaliti Eniko ambaye kwa sasa amebeba ujauzito wa mtoto wao wa kwanza.

Katika video hiyo Kevin Hart ameonekana akiwa na wanawake wawili ndani ya gari nje ya ufukwe wa Miami Hotel katika majira ya 5:00. Taarifa zimedai kuwa Hart baadae alishiriki kimapenzi na wanawake hao.

Mara baada ya skendo hiyo kuvuma mitandaoni huku wengi wakilaani kitendo cha mchekeshaji huyo kumsaliti mkewe, Hart amejibu tuhuma hizo kwa kutuma meme yake mwenye akicheka katika mtandao wa Instagram huku ikiandikwa “At the end of the day, you just gotta laugh at the BS”

 

#LiveLoveLaugh …..SMDH

A post shared by Kevin Hart (@kevinhart4real) on

Kevin na Eniko walifunga ndoa mnamo August mwaka 2015 na walitangaza kutarajia kupata mtoto hapo May mwaka huu.

Continue Reading

More in Mahusiano

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top