Connect with us

Michezo

Dangote ahahidi kumfukuza Wenger akifanikiwa kuinunua Arsenal

Dangote / tiririkablog.com

Bilionea wa Nigeria na raisi wa Dangote Group, Aliko Dangote, amerudisha tena mpango wa kuinunua klabu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza, Arsenal.

Dangote amesema atatoa ofa kwa mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke mara baada ya ujenzi wa kiwanda chake cha kusafisha mafuta mjini Lagos utakapomalizika.

Bilionea huyo na mfanyabiashara mkubwa amekuwa akiishabikia klabu ya Arsenal tangu miaka ya 1980 na utajiri wake una thamani ya paundi bilioni 8.6

Dangote aliiambia Bloomberg kuwa jambo la kwanza atakalobadilisha katika klabu hiyo ni kocha, na aliweka wazi kuwa anafahamu amefanya makubwa lakini ni muda wa mtu mwingine kujaribu bahati yake.

Mapema mwaka huu mmiliki wa klabu hiyo Kroenke alitupilia mbali ofa ya paundi bilioni moja kutoka kwa Alisher Usmanov.

Continue Reading

More in Michezo

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top