Connect with us
Coutinho / tiririkablog.com

Michezo

Liverpool waitolea nje ofa ya tatu ya Barcelona kwa Coutinho

Klabu ya Liverpool imeendelea kutia ngumu kumuachia kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Philipe Coutinho kwenda kujiunga na klabu ya Barcelona.

Barcelona ambao bado wanahaha kutafuta mbadala wa Neymar aliyejiunga na PSG kwa rekodi ya dunia, imetuma dau lililotajwa kufikia euro milioni 125 (sawa na paundi milioni 114).

Licha ya dau hilo kuwa kubwa mno bado klabu ya Liverpool imegoma kulikubali na kuifanya kuwa ofa ya tatu kutoka kwa miamba ya Hispania kukataliwa.

Bado Barcelona inategemewa kupanda dau zaidi kutokana na uwezekano mkubwa wa mbrazili huyo kuihama klabu yake ya Liverpool msimu huu mara baada ya kuomba kuruhusiwa kuondoka mapema mwezi huu.

Coutinho tayari amekosa mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Watford na mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Hoffenheim na pia ataikosa mechi ya pili ya ligi kuu dhidi ya Crystal Palace hapo Jumamosi.

Continue Reading

More in Michezo

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top