Connect with us
Daniel Craig, James Bond / tiririkablog.com

Filamu & TV

Muigizaji Daniel Craig kuendelea kuwa nyota wa James Bond

Daniel Craig, James Bond / tiririkablog.com

Kwa takribani baada ya miaka miwili hatimaye muigizaji mashuhuri wa filamu za James Bond, Daniel Craig amethibitisha kurudi tena kuigiza toleo lingine la filamu hizo.

Muigizaji huyo kwa muda mrefu alionekana kutokuwa muwazi juu ya hatma yake kuhusu kuendelea kuwa muigizaji mkuu wa filamu za Bond licha ya kupewa ofa nono ya kurudi tena kuigiza.

Mnamo mwaka 2015, Craig alimuambia muandishi mmoja kuwa yuko tayari kuvunja glass na kuchana kifundo cha mkono wake kuliko kurejea kuigiza tena kama James Bond.

Hata hivyo katika mahojiano na kipindi cha  The Late Show with Stephen Colbert alivyoulizwa kama atarudi kuendela kuigiza tena filamu hizo, aliafiki na kusema ndio.

Continue Reading

More in Filamu & TV

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top