Connect with us
usher-laura

Majuu

Binti aliyemshtaki Usher matatani baada ya simu yake kurekodiwa

Ushahidi mpya umewekwa wazi kwenye skendo inayomkabili mwanamuziki Usher kuhusu kuambukiza wanadada ugonjwa wa zinaa (Herpes).

Mwanadada Laura Helm alikuja na madai mwezi uliopita ya kuwa nae aliambukizwa na mwanamuziki huyo  na kumshtaki huku akidai alipwe dola za Marekani milioni 20.

Katika tamko alilolitoa mwanzo mwanadada huyo alisema kuwa yeye na Usher hawakutumia kondomu mara ya pili walivyokutana kimwili, jambo linalomfanya aamini aliambukizwa virusi hivyo visivyotibika.

Hata hivyo, katika mazungumzo ya simu yaliyorekodiwa na kudakwa na TMZ, Laura alisikika akisema wawili hao walikuwa wakitumia kinga mara zote walizokutana kimwili.

Pia katika mazungumzo hayo yaliyorekodiwa, Laura alisikika akisema hana nia ya kumshtaki mwanamuziki huyo lakini baada ya siku mbili mwanadada huyo alifanya hivyo.

Tayari mazungumzo hayo yametia shaka madai ya mwanadada huyo dhidi ya Usher na huenda yakatupiliwa mbali.

Kwa sasa Laura na wanadada wengine wawili ndio wanaomshtaki staa huyo wa No Limit kwa madai kuwa amewaambukiza ugonjwa wa zinaa.

 

 

 

Continue Reading

More in Majuu

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top