Connect with us

Mastaa

Mapenzi ya Jhene Aiko kwa Big Sean yapamba moto, achora tattoo yake

Mapenzi ya Jhene Aiko kwa Big Sean yapamba moto, achora tattoo yake

Mapenzi ya mastaa mara nyingi huwa sio ya kudumu lakini kwa mwanadada Jhene Aiko huenda ikawa ni tofauti mara baada ya kuamua kuchora tattoo kubwa ya uso wa mpenzi wake Big Sean mkononi.

Mchoraji wa tattoo hiyo Miryam  “The Witchdoctor” Lumpini ametuma picha katika ukurasa wake wa Instagram ikionesha mkono wa Jhene Aiko ukiwa na tattoo hiyo mpya ya uso wa rapa Sean.

Mkono wa Jhene Aiko

Lumpini aliandika ujumbe chini ya picha hiyo uliosomeka,  “Art is ❤️thanks Jheńe for allowing me to share this moment.” Akionesha furaha yake kwa kupewa nafasi ya kumchora mwanamuziki huyo maarufu.

Wiki iliyopita Aiko alikamilisha taratibu za talaka na mtayarishaji wa muziki Dot Da Genius, wawili hao walikuwa wametengana tangu mwaka jana na kutoa mwanya kwa Sean kuwa na mwanadada huyo tangu kipindi hicho.

 

Continue Reading

More in Mastaa

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top