Connect with us
Messi - tiririkablog.com

Michezo

Maajabu ya Messi yaipeleka Argentina Kombe la Dunia, Chile yatolewa

Maajabu ya Messi yaipeleka Argentina Kombe la Dunia, Chile yatolewa

Lionel Messi ameendelea kuonesha makali yake katika mchezo wa soka na mara hii makali yake hayo yaisaidia timu yake ya taifa ya Argentina kukata tiketi ya kuelekea Russia hapo mwakani.

Argentina ilikuwa kwenye hati hati ya kukosa tiketi ya kuelekea michuano hiyo mikubwa kabisa ya kimataifa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 47, lakini nahodha huyo aliweza kuiokoa timu yake dhidi ya timu ya Ecuador.

Ecuador ndio walianza kufungua lango la Argentina kupitia mchezaji Romario Ibarra kabla ya Messi hajashangaza umati katika jiji la Quito kwa kupiga hat-trick iliyoiwezesha timu yake kufuzu kwenda Kombe la Dunia.

Ibarra alifunga goli la kwanza mara baada ya sekunde 38 tu kwa kumalizia vizuri mpira uliomshinda golikipa namba mbili wa Manchester United Sergio Romero.

Messi alikuja kubadilisha mchezo kwa kusawazisha mnamo dakika ya 12 kwa kumalizia pasi safi aliyopewa na Angel Di Maria.

Staa huyo wa Barcelona alipiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja kwenye nyavu za juu mnamo dakika ya 20 na kumaliza kabisa mchezo kwa kufunga goli la tatu mara baada ya kuwachomoka mabeki watatu wa Ecuador na kubetua mpira uliomshinda golikipa.

 

Katika mechi nyingine, Chile ilikosa kufuzu katika michuano ya Kombe la Dunia kwa kukubali kipigo cha 3-0 dhidi ya Brazil katika mchezo uliogubikwa na rafu nyingi.

Argentina imemaliza kampeni katika michuano hiyo kufuzu kombe la dunia kwa kushika nafasi ya tatu, ikiweza kuruka nafasi tatu juu ya zaidi ambapo mwanzoni walikuwa katika nafasi ya sita.

 

 

Continue Reading

More in Michezo

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top