Connect with us
Salah

Michezo

Mohamed Salah afanya shule ibadilishe jina nchini Misri

Shujaa wa timu ya taifa Misri amefanya shule moja kutoka nchini humo kubadilisha jina na kupewa jina la shujaa huyo mara baada ya kuipeleka timu yake ya taifa katika michuano ya Kombe la Dunia.

Mshambuliaji huyo anayeichezea klabu kutoka nchini Uingereza Liverpool, alifunga magoli yote mawili katika mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Congo ulioisha kwa matokeo ya 2-1.

Mji aliokulia mchezaji huyo unaoitwa Basyoun umempa heshima hiyo kubwa kwa kuwezesha kulipeleka taifa lao katika mashindano hayo makubwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 28.

Gavana wa Gharbia Ahmed Deif ndiye aliyethibitisha kuwa shule aliyohitimu Salah imepewa jina lake kwa kuiwezesha nchi kwenda Russia hapo mwakani.

Pengine ni mwaka mzuri kwa mchezaji huyo kutokana na kuwa kwenye fomu nzuri tangu ajiunge na klabu yake ya Liverpool msimu huu na pia kwenye mechi za kufuzu kwenda Kombe la Dunia.

Continue Reading

More in Michezo

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top