Connect with us
Alikiba na Nandy

Bongo

Alikiba na Nandy wapeperusha vyema bendera ya Tanzania tuzo za Afrima

Bendera ya Tanzania imeendelea kupeperushwa vyema katika tasnia ya muziki mara baada ya wasanii wawili, Alikiba na Nandy kung’ara katika utoaji tuzo za All Africa Music Awards 2017 (AFRIMA).

Tuzo hizo zilizokuwa zikitolewa nchini Nigeria usiku wa kuamkia leo zilishuhudia wanamuziki hao kutoka Tanzania wakiibuka washindi katika vipengele mbalimbali vilivyotajwa katika tuzo.

Alikiba ama King Kiba aliibuka kidedea kwa kuondoka na tuzo mbili katika usiku huo ikiwemo Best Africa Collaboration kupitia ngoma ya Aje na ile ya Best Artist or Group in Africa RnB and Soul kupitia remix ya wimbo huo akimshirikisha M.I.

Kwa upande wa Nandy aliwatoa kimasomaso wasanii kike nchini kwa kuibuka mshindi wa tuzo ya  Best Female Artist In Eastern Africa Award ambayo pia ilikuwa ikiwaniwa na wasanii wengine kutoka Tanzania akiwemo Vanessa Mdee na Feza Kessy.

Continue Reading

More in Bongo

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top