Connect with us

Mastaa

Psquare waweka jumba lao la kifahari sokoni, nini tatizo?

Ndugu wanaounda kundi la Psquare kutoka Nigeria wameamua kufikia uamuzi wa kuuza mali zao zote wanazomiliki pamoja na jumba lao mashuhuri na la kifahari na kisha kugawana mali.

Jumba hilo maarufu linalojulikana kama Squareville limeonekana likiwa na bango linalotangaza kuuzwa na ndipo alipotafutwa ajenti na kuweka wazi kuwa mapacha hao wamefikia uamuzi huo.

Jumba limetajwa kuuzwa kwa fedha taslimu Naira milioni 320 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 2 za Kitanzania.

Psquare Squareville

Kwa nini wameamua kuuza mali zao wanazomiliki pamoja?

Uamuzi wa kuuza mali zao na kila mmoja kushika njia yake umekuja baada ya Peter kumshutumu kaka yao mkubwa, Jude, kuwa ametishia kumuua.

Peter amesema amechukua nafasi hiyo kufanya uamuzi mgumu wa kuvunja kabisa mkataba wake na kundi la Psquare.

Peter aliongeza kuwa yeye na mkewe wamekuwa wakitumiwa ujumbe wa kutishiwa maisha na kaingiwa na uoga juu ya maisha yake pamoja na familia.

Alisema Psquare haiwezi kuendelea tena na haimaanishi kuwa ana bifu na pacha wake Paul kwani undugu wao utaendelea kuwa pale pale.

Continue Reading

More in Mastaa

Tufuate Facebook

Trending

Advertisement
To Top